Uchimuzi wa Falsafa ya Ubuntu kama Mhimili wa Falsafa ya Waafrika katika Riwaya ya Bw. Myombekere na Bi. Bugonoka na Ntulanalwo na Buliwhali Juzuu ya 1

Abstract

Makala hii inalenga kujadili namna Falsafa ya Ubuntu inavyojichomoza kama mhimili wa Falsafa ya Waafrika katika riwaya ya Bw. Myombekere na Bi. Bugonoka na Ntulanalwo na Buliwhali Juzuu ya 1. Utafiti uliozaa makala hii ulikuwa wa kimaktaba. Mbinu ya uchambuzi matini ilitumika katika ukusanyaji wa data. Data zilizokusanywa zilichambuliwa na kuwasilishwa kwa kutumia mbinu ya usimbishaji wa maudhui. Nadharia ya Epistemolojia imetumika katika mchakato mzima wa ukusanyaji, uchambuzi na uwasilishwaji wa data. Makala inabainisha namna Falsafa ya Ubuntu inavyojitokeza kama mhimili wa Falsafa ya Waafrika kupitia miktadha mbalimbali ya maisha ya Waafrika. Miktadha hiyo ni: muktadha wa kufanya uamuzi binafsi na wa jamii nzima, muktadha wa ushirika katika kufanya shughuli mbalimbali za kijamii kama vile matatizo na sherehe, pamoja na muktadha wa kimahusiano baina ya mtu na jamii yake. Kwa kuzingatia mjadala uliofanywa, inapendekezwa kuwa tafiti zaidi zifanywe ili kubaini Falsafa Jumuifu ya Waafrika. Hii ni kwa sababu, mpaka sasa Falsafa ya Waafrika imekuwa ikitazamwa kupitia vipengele mbalimbali vya maisha ambavyo vinaibua mitazamo mbalimbali inayobainisha fikra za Waafrika kwa namna wanavyoutazama ulimwengu wao. Mitazamo hiyo, kwa mujibu wa makala hii, inaibua Falsafa ‘za’ Waafrika zinazoibuka kutoka katika kila kipengele na si Falsafa ‘ya’ Waafrika kama inavyotarajiwa kuwa.

Download

PDF

Keywords

epistemolojia
,
falsafa
,
falsafa ya Waafrika
,
Ubuntu
,
falsafa ya Ubuntu