Hotuba za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere: Mwangwi wa Semi za Kiswahili

Abstract

Makala hii inahusu namna hotuba za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (kuanzia hapa na kuendelea, atatajwa kama Mwalimu) zinavyoakisi semi za Kiswahili. Mwalimu ni Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Tanganyika, na baadaye Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hotuba zake zinahusu mambo aliyoyapa umuhimu kama vile uwajibikaji, uhuru, umoja, bidii katika kazi, uhusiano wa kimataifa, siasa ya ujamaa na kujitegemea, elimu, pamoja na malezi. Data zilizotumiwa katika makala hii zilikusanywa kutoka katika matini mbalimbali, zikiwamo hotuba, vitabu na kamusi za semi. Data hizo zilichambuliwa kwa njia ya uchambuzi matini. Kupitia hotuba hizo, imeonekana jinsi fasihi inavyoweza kuathiri namna ya mtu kufikiri, kunena, kutenda pamoja na kutazama hali ya maisha. Katika hotuba zake, semi za Kiswahili zimeakisiwa kwa namna mbili: ya moja kwa moja, ambapo anatumia semi kusisitiza jambo, na isiyo ya moja kwa moja, ambapo maudhui yake yanaoana moja kwa moja na semi za Kiswahili. Kwa jumla, kupitia namna zote mbili, imedhihirika kuwa kuna uhusiano kati ya fikra za Mwalimu na semi za Kiswahili. Hali hii inadhihirisha kuwa fasihi ni taaluma ambayo inagusa nyanja tofauti za maisha. Kwa hiyo, ni vema fasihi ifundishwe na kutafitiwa kwa kuhusianishwa na nyuga zingine zinazogusa maisha.

Download

PDF

Keywords

hotuba
,
semi
,
mwangwi