Uchambuzi wa Mbinu za Ukwezwaji wa Wahusika wa Riwaya Pendwa ya Kiswahili: Mifano kutoka Riwaya ya Njama na Kamata au Ua:

Abstract

Makala hii inachambua mbinu za ukwezwaji wa wahusika wa riwaya pendwa za Kiswahili. Ukwezwaji wa wahusika unajadiliwa kama mojawapo ya sifa bainifu za riwaya pendwa. Sifa hii inamaanisha kitendo cha kukipa kitu au mtu uwezo wa kiwango cha juu unaomwezesha kufanya jambo katika namna isiyo ya kawaida. Utafiti unaoripotiwa katika makala hii uliongozwa na Nadharia ya Umuundo inayojihusisha na suala la mjengeko wa matini (za kifasihi na zisizo za kifasihi). Data zilipatikana kwa njia ya kuchambua riwaya mbili zilizoteuliwa kimakusudi. Riwaya hizo ni Njama (1981) na Kamata au Ua (2020). Mbinu za ukwezwaji wa wahusika zilizobainika kutumiwa na waandishi wa riwaya teule ni: kuwavisha silika ya usangwini, kutumia sadfa, kuwavisha ujuzi wa juu wa kupigana, kuwapa uwezo mkubwa wa kufikiri, na kuwapa ujuzi wa hali ya juu wa kutumia teknolojia. Makala inapendekeza kuwa tafiti zingine zifanywe kuhusiana na vipengele vingine vya riwaya pendwa ya Kiswahili kama vile naratolojia, yaani sayansi ya usimulizi wa vitushi vya riwaya.

Download

PDF

Keywords

ukwezwaji
,
riwaya pendwa
,
wahusika
,
umuundo