Abstract
- Tafsiri ni muhimu sana kwa sababu inaunganisha watu wanaozungumza lugha tofauti. Majina ya pekee ya watu ni kipengele muhimu pia cha kutafsiriwa kwa sababu humbainisha mwenye jina na kuwasilisha ujumbe unaobebwa na mwenye jina hilo. Makala hii inatathmini tafsiri ya majina ya pekee ya watu kutoka Agano Jipya la Kiswahili kwenda Agano Jipya kwa Gᴉrᴉmi. Nadharia ya Ulinganifu wa Kimawasiliano imetumika katika tathmini hiyo. Data zilizotumika kwenye makala hii zimekusanywa kwa njia ya uchambuzi matini na usaili. Makala inaonesha kwamba mikakati inayotumika kutafsiri majina katika matini teule ni miwili ambayo ni unakilishaji na utohozi wa majina. Hata hivyo, unakilishaji sauti una dosari kadhaa kwa sababu ya kuhamishia fonolojia na mofolojia ya Kiswahili katika Gᴉrᴉmi. Pia, kuna upungufu katika tafsiri ya majina hayo ambao unatokana na kubadilishwa kwa sauti kusikotabirika, tafsiri kuegemea zaidi katika Kiingereza badala ya Kiswahili ambayo ni matini chanzi mama, na kukosekana kwa urari katika kutafsiri jina moja. Makala hii inapendekeza tafsiri ya majina ya pekee ya watu kutoka lugha moja kwenda nyingine kufanyika kwa usahihi na urari ili dhima inayobebwa na majina hayo iweze kuakisiwa katika matini lengwa.
Download
Keywords
Tafsiri
,majina ya pekee
,Gᴉrᴉmi
,Agano Jipya
