Mdhihiriko wa Kilongo cha Wanawake katika Jukwaa la Instagramu: Je, ni Mikakati ya Kujikomboa?

Abstract

Makala hii inabainisha namna kilongo cha wanawake katika jukwaa la Instagramu kinavyotumika kimkakati kuhamasisha wanawake kujikwamua kiuchumi, kijamii, na kielimu nchini Tanzania. Makala imeongozwa na mkabala wa kitaamuli kwa kutumia matini zilizochaguliwa kimakusudi kutoka katika jukwaa la Instagramu. Uchunganuzi wa data umeongozwa na Nadharia ya Uchanganuzi Tunduizi Kilongo. Data kutoka jukwaa la Instagramu zilikusanywa kwa njia ya uchanganuzi matini, ambapo sentensi, maneno, virai, tamathali za semi, semi mbalimbali, na kaulimbiu zilikusanywa kadri zilivyotumiwa na wanawake. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa uteuzi wa mtindo, ruwaza za kiisimu, na mada unaendana na mabadiliko ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na wanawake. Aidha, wanawake wanateua misamiati, sentensi, viambishi vya viwakilishi, tamathali za semi, kuchagiza umuhimu wa elimu kwa wanawake, ushujaa, uhuru wa kifedha, kujenga urafiki, na kuhamasisha mapambano dhidi ya hali zao duni. Pendekezo la makala hii ni kwamba, kwa vile utafiti huu ulihusisha wanawake tu, tafiti zingine zinaweza kufanywa zikijumuisha matumizi ya lugha kwa wanawake na wanaume katika mitandao ya kijamii.

Download

PDF

Keywords

Instagramu
,
kilongo
,
wanawake
,
jinsia
,
mtandaoni