Kutungamana kwa Itikadi na Propaganda katika Matini za Kifasihi

Abstract

Itikadi na propaganda ni dhana ambazo zimetungamana kila zinapojitokeza katika matini za kifasihi. Licha ya wataalamu mbalimbali kuonesha kuwa kuna uhusiano wa karibu kati ya itikadi na propaganda, hakuna utafiti ambao umefafanua sababu hasa za itikadi na propaganda kuonekana kutungamana kila zijitokezapo katika matini za kifasihi.  Hivyo, malengo ya makala hii: kwanza, ni kufafanua uhusiano uliopo baina ya itikadi na propaganda, kwa upande mmoja, na uhusiano wa dhana hizi dhidi ya fasihi, kwa upande mwingine. Pili, ni kufafanua sababu za propaganda na itikadi kujitokeza katika namna ya kutungamana katika matini za kifasihi. Nadharia ya Uhistoria Mpya ndio iliyotumika kufanikisha malengo ya makala hii. Hivyo, sababu zinazofanya itikadi na propaganda kutungamana ni pamoja na dhana ya itikadi inavyobainishwa, mashirikiano yaliyopo baina ya itikadi na propaganda katika kutawala au kudhibiti miundo ya diskozi kifani na kimaudhui, mbinu za propaganda zinavyofanya kazi, dhima au malengo ya propaganda, fasili ya itikadi na propaganda, mambo mawili yanayounganisha itikadi na propaganda, na mwisho ni uelezaji wa matukio au watendaji katika diskozi za kiitikadi.

Download

PDF