Uhawilishaji wa Fonimu za Kihehe na Athari zake katika Ujifunzaji wa Kiswahili Sanifu kama Lugha ya Pili

Abstract

Makala hii imechunguza uhawilishaji wa fonimu za Kihehe na athari zake katika ujifunzaji wa Kiswahili Sanifu kama lugha ya pili (L2). Data za makala hii zilikusanywa kutoka kwa wajifunzaji lugha jamii ya Wahehe ambao Kihehe ni lugha mama yao. Data za msingi za makala hii zilikusanywa kwa mbinu za masimulizi ya hadithi, uchambuzi wa nyaraka na jaribio lenye maswali ya orodha chunguzi. Uchambuzi sanifu wa data uliongozwa na nadharia ya Usasanyuzi Linganishi. Matokeo ya data za makala hii yanaonesha kuwa uhawilishwaji wa fonimu za Kihehe katika Kiswahili Sanifu, husababisha athari katika lugha hiyo. Athari zilizobainika ni urefushwaji wa matamshi ya maneno ya Kiswahili Sanifu; kuathiriwa kwa maana za maneno; na mabadiliko katika baadhi ya fonimu za Kiswahili Sanifu. Ili kuondoa au kupunguza athari hizo, makala hii imependekeza wajifunzaji lugha kupewa mazoezi ya kutosha ya somo la Kiswahili ambayo yatasaidia kupata maarifa zaidi ya lugha ya Kiswahili Sanifu.

Download

PDF