Uchapishaji na Usambazaji wa Istilahi za Sayansi Nchini Tanzania: Mifano kutoka Istilahi za Kiswahili za Biolojia, Fizikia na Kemia

Abstract

Lengo la makala hii ni kubainisha na kujadili kwa utondoti upungufu na athari za uchapishaji na usambazaji wa IS katika Kiswahili. Data zilizowasilishwa katika makala hii zimeibuliwa kutokana na udodosaji, usaili na mapitio ya nyaraka. Matokeo ya uchunguzi yanaonesha kuwa mfumo wa uchapishaji na usambazaji IS uliopo sasa katika Kiswahili una upungufu na   umesababisha athari kwa watumiaji wa istilahi hizo. Athari hizo ni: tofauti ya istilahi za watumiaji na zile za asasi za uundaji istilahi; ufundishaji wa somo la sayansi kuwa mgumu; wanafunzi kushindwa kujibu maswali katika mitihani yao ya sayansi; kuwapo kwa istilahi nyingi zisizotumiwa na watumiaji; na watumiaji kutumia IS zisizosanifishwa. Kwa kifupi, makala imetoa picha ya athari ya  IS zisipochapishwa na kusambazwa kwa watumiaji katika maeneo yao.

Download

PDF