Makosa ya Lugha katika Vyombo vya Habari Nchini Tanzania: Uchunguzi wa Televisheni

Abstract

Makala hii inalenga kuchanganua makosa ya lugha kwenye vyombo vya habari nchini Tanzania na kubainisha mbinu za kutatua makosa hayo. Data zilikusanywa kwa mbinu ya hojaji, mahojiano na usomaji wa matini za habari kutoka kwenye chaneli za TBC1, ITV na STAR TV. Nadharia ya Uchanganuzi Makosa imetumiwa kuchambua data na kuwasilisha matokeo ya utafiti. Aidha, utafiti umebaini makosa ya uchanganyaji wa misimbo, matumizi ya maneno yasiyostahili, utenganishaji na uunganishaji wa maneno isivyo, udondoshaji, uchopekaji, matamshi yasiyo sahihi, umoja na wingi, upatanisho wa kisarufi, mpangilio mbaya wa maneno na makosa ya kimantiki. Pia, makala imebaini kuwa makosa hayo yanaweza kutatuliwa kwa kutoa mafunzo ya lugha ya mara kwa mara kwa wanahabari, kutungwa kwa sheria ya kudhibiti matumizi ya lugha, kuhimiza utumiaji wa Kiswahili fasaha, kutumia wanataaluma wa lugha kwenye vyombo vya habari na kufanyika kwa uhariri wa kina. Hitimisho la makala hii ni kwamba makosa ya lugha katika vyombo vya habari nchini Tanzania yanahitaji tafiti nyingi na za kina ili kupata masuluhisho zaidi ya kuyaepuka kwa ustawi wa lugha ya Kiswahili.

Download

PDF