Sifa za Hofu katika Maisha ya Mwanadamu: Uchunguzi wa Mhusika Ngoma kutoka Riwaya ya Ua la Faraja

Uchunguzi wa Mhusika Ngoma kutoka Riwaya ya Ua la Faraja

Abstract

Kila mwanadamu mwenye uwezo wa kufikiri na kutafakari juu ya masuala mbalimbali yanayomzunguka huonesha hisia zinazoambatana na hali fulani katika kutoa maamuzi ya tafakuri yake. Moja kati ya hali zinazotawala fikra zake ni hofu. Kuwapo kwa hofu hubainika kupitia matendo ayafanyayo katika mazingira yanayomzunguka. Kimsingi, hofu humwongoza mwanadamu kuwa na maamuzi yanayosababisha kufanya au kutofanya jambo fulani. Kazi za kibunilizi, mathalani riwaya husawiri maisha halisi ya mwanadamu yanayofungamana na hali mbalimbali, ikiwamo hofu. Kwa msingi huo, makala hii inabainisha sifa za hofu kwa kumrejelea mhusika Ngoma kutoka riwaya ya Ua la Faraja. Data zilipatikana maktabani kwa kutumia mbinu ya usomaji matini. Vilevile, mbinu ya usaili ilitumika ili kupata data za kuthibitisha uhalisi wa sifa za hofu katika ulimwengu halisi wa mwanadamu. Misingi ya Nadharia ya Uhalisia imetumika katika uchunguzi, uchanganuzi na uwasilishaji wa matokeo ya utafiti. Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa katika riwaya ya Ua la Faraja kuna sifa kuu tatu za hofu: hofu hujizalisha kulingana na wakati, hofu huhusisha mlolongo wa wahusika wenye nasaba na hofu huibua tabia mpya kwa mwanadamu.

Download

PDF