Upungufu wa Tafsiri ya Lugha ya Ishara katika Wema Hawajazaliwa na Shetani Msalabani

Abstract

Tafsiri ni miongoni mwa taaluma zinazosaidia kurahisisha mawasiliano miongoni mwa watumiaji wa lugha tofauti. Taaluma hii imekuwa ikinufaisha taaluma nyingine kama vile sheria, utabibu na fasihi. Makala hii inajadili upungufu wa tafsiri ya lugha ya ishara katika Wema Hawajazaliwa na Shetani Msalabani. Hizi ni riwaya zilizotafsiriwa kwa Kiswahili kutoka katika riwaya ya The Beautyful Ones are Not Yet Born na Devil on the Cross za Ayi Kwei Armah na Ngugi wa Thiong’o, mtawalia. Aidha, Nadharia ya Ulinganifu wa Kimawasiliano imetumika kama kiunzi cha uchambuzi wa data zilizowasilishwa katika makala hii. Data za makala hii zimepatikana kwa kutumia mbinu ya usaili na uchambuzi wa matini.  Makala imebaini kuwa wafasiri wameonesha upungufu katika tafsiri ya lugha ya ishara. Upungufu huo umebainika kupitia vipengele vikuu ambavyo ni upotoshaji, udondoshaji, na tofauti za kiutamaduni. Makala inapendekeza kuwa wafasiri wa kazi za kifasihi wanapaswa kuzingatia misingi ya kiulinganifu katika kutafsiri lugha ya ishara ili kuwafanya wasomaji wao wapate ujumbe uliokusudiwa na waandishi wa matini chanzi.

Download

PDF