Sababu Zinazoukilia Matumizi ya Tungo za Utendeka na Utendwa katika Lugha ya Kiswahili

Abstract

Makala hii imechunguza tungo za utendeka na utendwa katika lugha ya Kiswahili. Hii ni kwa sababu, yapo madai miongoni mwa wanaisimu mbalimbali kwamba, tungo hizo zinafanya kazi inayofanana katika lugha kisarufi; yaani kupunguza kishiriki kimoja cha kitenzi katika muundo wa vishiriki vya kitenzi (Khamisi, 1972; Rugemalira, 1993; na Mkude, 2005). Data za utafiti huu zilipatikana kwa njia ya usomaji wa nyaraka pamoja na usaili. Uchanganuzi wa data umetumia misingi ya mkabala wa Sarufi Leksia Amilifu ulioasisiwa na na Bresnan na Kaplan mwishoni mwa miaka ya 1970. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba utendeka na utendwa ni tungo mbili tofauti kimuundo na kiuamilifu katika lugha ya Kiswahili. Aidha, imebainika kwamba ziko sababu kadhaa zinazoukilia utokeaji wa tungo hizo: muundo wa vishiriki vya kitenzi, upatanisho wa kisarufi, kuondoa mtenda katika tungo, umadaishaji wa kiathirika, ufokalishaji wa mtenda, ukwezaji wa mmiliki na kuondoa utata katika lugha. Kutokana na matokeo haya, inapendekezwa kwamba, utafiti zaidi kama huu ufanyike katika lugha nyingine za Kibantu ambazo hazijafanyiwa utafiti ili kulinganisha na kutofautisha sababu za utumikaji wake katika lugha ya Kiswahili na lugha lugha zingine za Kibantu.

Download

PDF