Mikakati ya Ushawishi wa Kisiasa katika Hotuba za Mgombea wa Kenya Kwanza 2022 Nchini Kenya

Abstract

Katika juhudi za kupata uungwaji mkono wa kisiasa, wagombea wa nyadhifa mbalimbali hutumia lugha yenye uwezo wa kuathiri fikra na hisia za wapiga kura ili kuwavutia na kushawishi kuwaunga mkono. Ni kutokana na hoja hii, utafiti uliozaa makala hii ulichunguza mikakati ya ushawishi wa kisiasa katika hotuba za kampeni za mgombea wa Muungano wa Kenya Kwanza katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2022 nchini Kenya. Utafiti uliongozwa na nadharia ya Uchanganuzi Hakiki wa Usemi. Sampuli ya kimakusudi ilitumiwa kuteua hotuba ishirini za mgombea wa Muungano wa Kenya Kwanza. Data zilikusanywa kwa kusikiliza kwa umakini hotuba zilizopakuliwa kutoka jukwaa la YouTube. Uchanganuzi wa data na uwasilishaji wa matokeo ulifanywa kinathari. Matokeo yalibainisha kwamba mgombea alitumia ufifishaji, dhanio, na kidokezo ili kuhalalisha ajenda yake kama mwanasiasa mwadilifu aliyefaa kupewa nafasi ya uongozi. Makala hii itachangia kupanua tasnia ya isimu kwa kuongeza maarifa katika taaluma ya pragmatiki. Pia, itaongeza mchango katika sajili ya siasa kwa kuweka wazi jinsi wagombea wa nyadhifa za kisiasa wanavyotumia hotuba kuuza sera na kuimarisha ajenda zao ili kupata mamlaka. Halikadhalika, itaufaa umma unapofanya uamuzi katika changuzi za kisiasa.

Download

PDF

Keywords

hotuba
,
itikadi
,
mamlaka
,
ushawishi wa kisiasa