Usawiri wa Utandawazi katika Riwaya za Kisasa za Kiswahili: Mifano kutoka Babu Alipofufuka (2001) na Makuadi wa Soko Huria (2002)

Abstract

Makala hii inalenga kubainisha vipengele mbalimbali vya utandawazi vinavyojitokeza katika riwaya za kisasa za Kiswahili. Riwaya teule zilizotumika wakati wa ukusanyaji wa data na uchanganuzi wake ni Babu Alipofufuka (2001) na Makuadi wa Soko Huria (2002). Riwaya hizi zimeteuliwa kwa kuwa ziliandikwa kati ya mwaka 2000 hadi 2010 kipindi ambacho utandawazi ulizungumziwa na wanazuoni wengi katika fasihi ya Kiswahili na hata nje ya fasihi. Pia, riwaya teule zinaakisi vizuri hali halisi ya utandawazi hapa nchini. Data za makala hii zilipatikana kwa kutumia mbinu ya usomaji makini wa matini katika riwaya teule za kisasa za Kiswahili. Aidha, data zilichambuliwa kwa kutumia mkabala wa kitaamuli, ambapo maelezo yalitumika kuwasilisha uchambuzi wa data. Nadharia ya Uhalisia imetumika katika uchambuzi wa data na uwasilishaji wake. Utafiti ulibaini vipengele mbalimbali vya utandawazi vilivyojitokeza katika riwaya teule za kisasa za Kiswahili. Navyo ni: kushamiri kwa uwekezaji, umilikishwaji wa ardhi, kushamiri kwa ubinafsishaji, kuingizwa kwa utamaduni wa kigeni na ukwepaji wa kodi. Aidha, tunapendekeza tafiti nyingine zifanyike kuhusu ulinganisho kifani au kimaudhui katika riwaya za kisasa za Kiswahili na riwaya zilizoandikwa kabla ya utandawazi.

Download

PDF

Keywords

Utandawazi
,
riwaya za kisasa